

Lugha Nyingine
感冒有什么症状
Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi, ambaye pia ni Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), akikutana na ujumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Baraza la Biashara la Marekani na China mjini Beijing, mji mkuu wa China, Julai 30, 2025. (Xinhua/Gao Jie)
BEIJING - China na Marekani zinapaswa kuheshimu maslahi makuu na makubwa ya kila upande, na kuepuka kuangukia katika makabiliano na migogoro, Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi amesema jana Jumatano mjini Beijing, Mji Mkuu wa China alipokutana na ujumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Baraza la Biashara la Marekani na China (USCBC).
Ametoa wito kwa pande hizo mbili kuanzisha njia zaidi za mawasiliano na mashauriano, kutendeana kwa mtazamo wa uhalisia, wenye mantiki na wa kivitendo, na kujenga hisia sahihi za kimkakati.
Wang, ambaye pia ni Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) amesema, haijalishi namna gani hali inavyobadilika, China imekuwa ikidumisha mwendelezo na utulivu wa sera yake kuhusu Marekani, na China itashughulikia na kusukuma mbele uhusiano wake na Marekani kwa kufuata kanuni tatu: kuheshimiana, kuishi pamoja kwa amani na ushirikiano wenye manufaa kwa pande zote.
“China inapenda kuimarisha mawasiliano na Marekani ili kuepusha maamuzi ya kimakosa, kudhibiti tofauti, kutafuta fursa za ushirikiano, kutekeleza maafikiano yaliyofikiwa kati ya wakuu wa nchi hizo mbili, na kuhimiza maendeleo imara, mazuri na endelevu ya uhusiano kati ya China na Marekani” ameongeza.
Pia amehimiza kutilia maanani kanuni za kuheshimu, usawa na kulipizana kwa usawa na kujiepusha na umwamba wa upande mmoja, akitoa wito wa kufanya mambo makubwa, ya kivitendo na mazuri zaidi kwa manufaa ya nchi hizo mbili na dunia nzima.
Wang amesema kuwa China itapanua ufunguaji wake mlango wa ngazi ya juu na kujenga mazingira ya biashara ya daraja la kwanza yenye mwelekeo wa soko, yanayozingatia sheria na ya kimataifa.
"China inatumai kuwa kampuni za Marekani yataendelea kuwa na matumaini kuhusu China na kuwekeza ndani ya nchi ili kupata kunufaishana na ukuaji wa pamoja," ameongeza.
Ujumbe huo ulijumuisha Mwenyekiti wa Bodi ya USCBC Rajesh Subramaniam; Mwenyekiti wa Thermo Fisher Scientific Marc N. Casper; Mwenyekiti wa Otis Worldwide Corporation Judy Marks; Rais na Afisa Mkuu Mwendeshaji wa Goldman Sachs John E. Waldron; Makamu wa Rais Mwandamizi wa Kampuni ya Boeing na Rais wa Boeing Global Brendan Nelson; mwanzilishi na Makamu Mwenyekiti wa United Family Healthcare Roberta Lipson; Afisa Mwendeshaji Mkuu wa Apple Inc. Sabih Khan; na Rais wa USCBC Sean Stein.
Wamesema uhusiano kati ya Marekani na China ni uhusiano muhimu zaidi wa pande mbili duniani hivi sasa, na kwamba mawasiliano mazuri na yenye mtazamo wa mbali kati ya wakuu wa nchi hizo mbili yametoa mwongozo na msukumo wa kustawisha uhusiano wa pande mbili.
Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi, ambaye pia ni Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), akikutana na ujumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Baraza la Biashara la Marekani na China mjini Beijing, mji mkuu wa China, Julai 30, 2025. (Xinhua/Gao Jie)
Mandhari ya Kipekee ya Karst katika Mkoa wa Guizhou yavutia watalii
Tamasha la kimataifa la densi lafunguliwa katika Mkoa wa Xinjiang, China likiwa na maonyesho 52
Wakulima wa China wawa na pilikapilika za uzalishaji wa kilimo katika kipindi cha Dashu
Maliasili nyingi za chumvi zaongeza mapato ya wanakijiji katika Wilaya ya Gegye, Xizang, China
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma